• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi mmoja auawa na wawili kujeruhiwa katika shambulizi la kundi la Al-Shabaab nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-11 19:09:08

    Afisa mmoja wa polisi ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye gari waliyokuwa wakisafiria baada ya kukanyaga bomu katika kaunti ya Lamu jana jioni.

    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani Larry Kieng leo amethibitisha tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Mararani, akisema maafisa watano wa polisi bado hawajulikani walipo baaada ya shambulio hilo. Kieng amefafanua kuwa gari hiyo ambayo ni ya kitengo cha doria ya mpakani iliondoka Jumapili kufanya doria ikiwa na askari 12 wakiongozwa na Inspekta wa Polisi Boniface Maduli. Amesema baada ya mlio wa bomu kusikika polisi waliondoka kituoni kwa miguu kwenda kujua kilichotokea. Kamanda Kieng amethibitisha kuwa gari lilikanyaga bomu na kufuatiwa na mashambulizi ya risasi. Katika shambulizi hilo Inspekta madilu aliuawa na wengine wawili kupelekwa kambi ya Manda kwa matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako