• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Hazina inataka kuwa na usemi kwa kodi za kaunti

  (GMT+08:00) 2017-09-11 20:18:03

  Kaunti zote zinapaswa kuwasilisha mapendekezo ya kodi kwa Hazina ya Taifa na Tume ya Ugawaji wa Mapato (CRA) miezi 10 kabla ya mwanzo wa mwaka wa fedha, kwa sababu Serikali inajianda kumaliza kodi za ndani zisozo na msingi maalum.

  Sheria iliyopendekezwa ilichapishwa kwa ukaguzi wa umma wiki iliyopita, na kama itapitishwa, kaunti zote zitalazimika kutambua mamlaka yao ya kukusanya kodi.

  Takwimu kutoka kwa Mdhibiti wa Bajeti (COB) ya miezi tisa, ya mwaka ulioisha Juni 30 inaonyesha kwamba jumla ya fedha walipata kutoka kwa kaunti 47 Sh bilioni 24.71, ambayo ilikuwa asilimia 41.4 ya lengo la kila mwaka la Sh bilioni 59.71.

  Mdhibiti Agnes Odhiambo anaelezea kuwa hali imeshuka ikilinganishwa na sh bilioni 25.89 sawa na asilimia 46.9% ya mwaka wa fedha wa 2015/16 mapato ya kila mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako