• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu maalum ya uchunguzi kuanza uchunguzi kuhusu mgodi wa madini wa Mwadui

    (GMT+08:00) 2017-09-12 09:15:23

    Timu maalum imeanza uchunguzi kuhusu shughuli za uzalishaji na biashara katika mgodi wa madini wa Mwadui unaomilikiwa na kampuni ya Williamson Diamonds, mkoani Shinyanga.

    Uchunguzi huo unafuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli wa Tanzania kwa idara za ulinzi na usalama, kuwafanyia uchunguzi maofisa waandamizi waliotajwa kwenye ripoti mbili za bunge la Tanzania, kuhusu uchimbaji wa madini ya almasi na Tanzanite.

    Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bibi Zainab Terack amesema timu ya wachunguzi inahusisha maofisa wa idara za ulinzi na usalama, na kuanzia jumapili mgodi wa Williamson Diamonds umefungwa, ili kupisha uchunguzi dhidi ya maofisa wanaosimamia uchimbaji, tathmini na usafirishaji wa almasi.

    Wiki iliyopita Waziri wa fedha wa Tanzania Dr. Philip Mpango pia aliamuru kutaifishwa kwa mali za maofisa waliochangia kulitia hasara taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako