• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya Marekani yarudisha kwa muda zuio la wakimbizi la Rais Trump

    (GMT+08:00) 2017-09-12 09:15:45

    Mahakama kuu ya Marekani jana imeidhinisha ombi kutoka kwa serikali ya Rais Donald Trump kurudisha kwa muda zuio la wakimbizi wanaotaka kuingia nchini Marekani.

    Kwenye amri ya muda mfupi iliyosainiwa na Jaji Anthony Kennedy, mahakama inazuia kwa muda zuio lililotolewa na mahakama kuhusu amri ya Rais Trump kupiga marufuku wakimbizi walioko kwenye mipango ya serikali ya Marekani kuingia Marekani.

    Wiki iliyopita mahakama ya Marekani pia iliizuia serikali ya Marekani kupiga marufuku bibi na babu, wajomba na shangazi na ndugu wengine wa watu walioko Marekani kuingia Marekani.

    Zuio la Rais Trump kwa wakimbizi kutoka baadhi ya nchi, lilitolewa kwa madai kwamba serikali inahitaji muda wa kufanya ukaguzi wa nani aruhusiwe kuingia Marekani. Mahakama kuu ya Marekani inasubiri kusikiliza maoni ya serikali mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako