• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNEP latoa ripoti ya kwanza kuhusu utajiri wa kiikolojia eneo la jangwa

    (GMT+08:00) 2017-09-12 09:47:58

    Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limetoa Ripoti ya tathmini kuhusu utajiri wa kiikolojia wa Jangwa la Kubuqi nchini China kwenye mkutano wa 13 wa washiriki wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu udhibiti wa jangwa, ikiwa ni ripoti ya kwanza kuhusu utajiri wa kiikolojia kutolewa na Umoja wa Mataifa.

    Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Jangwa la Kubuqi nchini China limezalisha mali za kiikolojia zenye thamani zaidi ya dola bilioni 76.6 za kimarekani, kuwaondoa wenyeji zaidi ya laki moja kutoka kwenye umaskini, na kutoa nafasi zaidi ya milioni moja za ajira.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la UNEP Bw Erik Solheim amesema, Jangwa la Kubuqi la China limekuwa mfano wa kuigwa wa kuunganisha maendeleo ya kiuchumi na juhudi za kuondoa umaskini, ambao umetoa uzoefu muhimu duniani kuhusu udhibiti wa jangwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako