• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuanza kusimamia lengo la sita la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2017-09-12 10:19:44

  Katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji ya Kenya Bw. Fred Segor amesema, nchi hiyo itaanza kusimamia lengo la sita la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa, linalolenga kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kunywa na miundombinu ya afya kwa watu wote hadi kufikia mwaka 2030.

  Bw. Segor amesema hayo katika mkutano wa maji uliofanyika huko Nairobi, huku akiongeza kuwa Kenya imechaguliwa na shirika la maji la Umoja wa Mataifa kufanya majaribio ya kusimamia na kuripoti kuhusu lengo hilo.

  Bw. Segor amesema ili kufanikiwa kusimamia lengo hilo la Umoja wa mataifa, Kenya itashirikiana na washirika wa ndani na wa kimataifa ambao wametoa njia zenye uvumbuzi za kuripoti zinazozingatia maendeleo ya kiteknolojia.

  Pia amesema, wanawataka wadau wote wahusika kuunga mkono na kuzidisha usimamizi na ripoti kwa maji na miundombinu ya afya kutoka ngazi ya kaunti hadi taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako