• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya mambo ya nje ya China yazungumzia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio kuhusu Korea Kaskazini

  (GMT+08:00) 2017-09-12 18:51:21

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang alipojibu swali kuhusu baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa kupitisha azimio namba 2375 kuhusu majaribio ya nyuklia ya Korea Kaskazini, amesema China inaunga mkono baraza la usalama kuchukua hatua zinazohitajika.

  Msemaji huyu amesema Korea Kaskazini imefanya majaribio tena bila kujali upinzani wa jumuiya ya kimataifa, na imekwenda kinyume na maazimio husika ya baraza la usalama.

  Jana baraza la usalama lilipitisha kwa kauli moja azimio linaloonesha msimamo wa pamoja wa wajumbe wa baraza hilo kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea na kanda hiyo, kusukuma mbele mchakato wa kuondoa silaha za nyuklia kwenye peninsula hiyo, na kulinda mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia wa kimataifa. China inatarajia kuwa azimio hilo litatekelezwa kikamilifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako