• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamilioni ya wapalestina watoa wito kutatua suala la Israel na Palestina kwa njia ya amani

  (GMT+08:00) 2017-09-12 18:04:23

  Mwenyekiti wa shirika la amani la Palestina la CAWS Bw Walid Assaf amekabidhi barua yenye mamilioni ya saini ya wapalestina kwa rais wa nchi hiyo Mahmoud Abbas ambayo inatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuisaidia kusimamisha ukaliaji wa Israel nchini humo na kujenga taifa huru la Palestina.

  Bw. Assaf amesema, barua hiyo inalenga kutoa wito kuharakisha Palestina na Israel kutimiza amani na kuanzisha nchi huru ya Palestina na kueleza matarajio ya amani ya wapalestina.

  Habari zinasema Bw. Abbas amekubaliana na pendekezo la Bw Walid Assaf, na atakabidhi barua hiyo kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres atakapohudhuria mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako