• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za COMESA zatakiwa kuwa na sera bora kwa sekta ya madini

  (GMT+08:00) 2017-09-12 18:49:53

  Katibu mkuu wa muungano wa soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) bwana Sindiso Ngwenya ametoa wito kwa nchi wanachama kuharakisha uwianishaji wa sera kwenye sekta ya uchimbaji madini ili kuifanya sekta hiyo kuwa na ushindani na kuzalisha faida zaidi.

  Ngenya amesema uwezo kamili wa sekta hiyo unaweza kufikiwa tu ikiwa kutakuwa na mifumo bora ya usimamizi na kufuata makubaliano ya kibiashara ya kimataifa yaliopo kwa sasa.

  Ngwenya amesema kukiwa na mifumo bora ya taasisi husika itawezesha COMESA kuwa na sauti kuhusu maamuzi ya madini yaliopo kwenye kanda hiyo.

  Mwaka 2014, COMESA ilitia saini mkataba wa maelewano na serikali ya Australia katika sekta ya madini, petrol, kilimo, utoaji wa mafunzo na kujenga uwezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako