• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Kenya kujenga barabara ya laini sita kati ya Nairobi na Mombasa

  (GMT+08:00) 2017-09-12 18:51:14

  Kampuni ya Bechtel International Inc ya Marekani imepewa kandarasi ya kujenga barabara kuu ya laini 6 kutoka Mombasa hadi Nairobi.

  Mkurungezi wa ujenzi wa mamlaka ya ujenzi wa barabara Peter Mundinia amesema mradi huo wa kilomita 473 itaungana na ile iliopendekezwa ya Nairobi-Nakuru-Mau Summit na hivyo kuunganisha bandari ya Mombasa na Malaba katika mpka wa Kenya na Uganda.

  Barabara hiyo itajengwa kwa gharama ya dola bilioni 2.1.

  Uganda tayari inajenga barabara kuu kutoka mji mkuu Kampala-Jinja ambayo ni sehemu ya ushoroba wa kaskazini.

  Itakapokamilika, miradi hiyo ndani ya miaka 6 ijayo itahimarisha ushindani wa kibiashara sio Kenya na Uganda tu lakini pia Rwanda, Burundi na D R Congo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako