• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaipatia Kenya msaada wa kifaa cha utabiri wa hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-09-12 18:51:55

    Wizara ya mazingira ya Kenya imepokea msaada wa kifaa cha utabiri wa hali ya hewa kinachojiendesha kutoka kwa China, ikiwa ni sehemu za juhudi za Kenya kuboresha huduma zake za utabiri wa hali ya hewa.

    Waziri wa mazingira na maliasili Profesa Judy Wakhungu, amesema kwenye sherehe ya kupokea msaada huo kuwa, kifaa hicho kitasaidia kuinua uwezo wa Kenya wa kutabiri na kuripoti kwa wakati mwenendo wa hali ya hewa.

    Balozi wa China nchini Kenya Bw Liu Xianfa alihudhuria sherehe hiyo, na kusema msaada huo umeweka njia ya kuimarisha ushirikiano kati ya serikali ya China na Kenya kwenye utabiri wa hali ya hewa, kilimo na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Ofisa mwandamizi wa mamlaka ya hali ya hewa ya Kenya Bw Samuel Mwangi amesema msaada huo wa China umeboresha ukusanyaji na utoaji wa habari kuhusu hali ya hewa nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako