• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Huenda serikali ya Tanzania ikatwaa umiliki wa mgodi wa almasi unaomilikiwa na kampuni Uingereza

  (GMT+08:00) 2017-09-12 18:52:57

  Huenda serikali ya Tanzania ikatwaa umiliki wa mgodi wa almasi unaomilikiwa na kampuni moja ya Uingereza- Petra Diamond Ltd, baada ya rais John Magufuli kuagza kuchunguzwa kwa kandarasi iliopewa kampuni hiyo.

  Uchunguzi wa bunge umebaini kuwa kuna udanganyifu mkubwa kupendekeza, miongoni mwa mambo mengine, kutwaliwa kwa wa mgodi huo, pendekezo ambalo lilikubaliwa kwa haraka na Rais Magufuli.

  Spika wa bunge Job Ndugai mwezi juni aliunda kamati mbili za bunge kutathmini jinsi Tanzania inavyonufaika na madini ya almasi na tanzanite.

  Kamati hizo zilichunguza maswla kama vile umiliki, uchimbaji na kanuni za sekta hiyo na kuwasilisha ripoti bungeni septemba 6.

  Baada ya kupokea ripoti hiyo rais Magufuli aliagiza kubadilishwa kwa sheria zote za uchimbaji ili kuziba mianya iliopo.

  Tanzania ni mojawepo wan chi zenye madini mengi ya almasi barani Afrika lakini kutokuwepo na sheria za kthibiti uchimbaji na uuzaji, manufaa ya madini hayo hayajasaidia uchumi wa taifa vilivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako