• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 13 wa washiriki wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu udhibiti wa jangwa wafungwa

    (GMT+08:00) 2017-09-13 09:43:02

    Mkutano wa 13 wa washiriki wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu udhibiti wa jangwa umefungwa jana mjini Ordos mkoani Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China.

    Habari zinasema kwenye mkutano huo, washiriki wameelewa zaidi madhara ya kupanuka kwa jangwa, kutoa mapendekezo ya kukabiliana na ukame na dhoruba ya vumbi, na kuhakikisha kazi za pande husika kwenye sekta za kuhimiza udhibiti wa jangwa na kutimiza lengo la kutopanuka kwa jangwa kote duniani ifikapo mwaka 2030.

    Kwenye hafla ya kufunga mkutano, katibu mtendaji wa idara ya udhibiti wa jangwa ya Umoja wa Mataifa Bibi Monique Barbut amempatia mkuu wa idara kuu ya misitu la China Bw Zhang Jianlong tuzo ya kutoa mchango mkubwa katika udhibiti wa jangwa. Bi Monique amesema China imeipatia dunia mfano wa kuigwa kwenye kudhibiti kuenea kwa jangwa, teknolojia na mfumo wa China vimetoa mchango mkubwa katika kutimiza lengo la kudhibiti kupanuka kwa jangwa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako