• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi wanaorudi Somalia kwa msaada wa umoja wa mataifa wafikia elfu 72

    (GMT+08:00) 2017-09-13 09:50:45

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR limesema limewarudisha kwa hiari wakimbizi elfu 72 kutoka kwenye kambi za wakimbizi nchini Kenya tangu kazi hiyo ianze mwaka 2014.

    Taarifa iliyotolewa mjini Nairobi inasema wakimbizi 70,202 wamerudishwa kutoka kambi ya Dadaab na wengine 1,899 kutoka kambi ya Kakuma.

    UNHCR imesema kwa sasa kuna wakimbizi 17,478 ambao wamejiandikisha kurudi kwa hiari.

    Hata hivyo dawati la wakimbizi wanaojiandikisha limesema idadi ya wakimbizi wanaojiandikisha kurudi kwa hiari imepungua, hasa kutokana na kurudisha kwa wakimbizi kwa njia ya barabara kumesimamishwa, na mji wa Baidoa umesimamisha kupokea wakimbizi.

    Inakadiriwa kuwa watu milioni 1.1 ni wakimbizi wa ndani nchini Somalia, na wengine laki 9 ni wakimbizi nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako