• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sheria ya kwanza kuhusu Brexit yapita kikwazo cha bunge

  (GMT+08:00) 2017-09-13 09:51:07

  Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amepata ushindi kwenye mswada wa sheria muhimu inayotandika njia ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

  Baada ya mjadala wa saa tatu kwenye baraza la chini la bunge la Uingereza na kufuatiwa na upigaji kura, mswada huo ulipitishwa kwa kura 17. Hata hivyo ushindi huo wa chama cha wahafidhina ungepungua, kama wabunge saba wa chama cha leba, wasingekaidi agizo la kiongozi wa chama cha Leba Bw. Jeremy Corbyn kuupigia kura ya hapana.

  Mswada uliopitishwa ni ule unaohusu kufanya sheria za miaka 40 za Umoja wa Ulaya kufanya kazi nchini Uingereza baada ya kujitoa umoja wa Ulaya mwaka 2019.

  Wakati huo huo duru ya nne ya mazungumzo kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya imepangwa kufanyika tarehe 25 Septemba. Vyombo vya habari vya Uingereza vimesema waziri mkuu Bibi Theresa May anatarajiwa kutoa hotuba muhimu kuhusu kujitoa Umoja wa Ulaya siku tatu kabla ya mazungumzo hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako