• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya AfDB yaipongeza Ethiopia kwa kutumia fedha katika miradi ya maendeleo

  (GMT+08:00) 2017-09-13 10:06:41

  Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imeipongeza Ethiopia kwa kutumia fedha katika miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

  Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo kanda ya Afrika Mashariki Bw. Calleb Weggoro ambaye amefanya ziara nchini Ethiopia, kukagua miradi ya usafiri na nishati iliyogharimiwa na benki hiyo kwenye ushoroba kati ya Ethiopia na Kenya.

  Taarifa iliyotolewa na benki hiyo inasema, baada ya ziara hiyo Bw. Weggoro aliipongeza serikali ya Ethiopia kwa kushirikiana haraka na ofisi za benki hiyo nchini Ethiopia kuwaleta wakandarasi wapya ya utekelezaji, wanaotarajiwa kukamilisha kazi mwishoni mwa mwaka 2018.

  Mbali na mradi wa nishati kati ya Kenya na Ethiopia, Benki ya AfDB pia inachangia katika mradi wa usambazaji wa umeme kutoka Ethiopia hadi Djibouti. Miradi hiyo itailetea Ethiopia fedha za kigeni kupitia mauzo ya bidhaa za nishati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako