• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania na Kenya kuendesha mazungumzo ya biashara Novemba

  (GMT+08:00) 2017-09-13 10:10:09

  Kenya na Tanzania zitafanya mazungumzo mwezi Novemba ili kuimarisha biashara kati ya pande hizo mbili.

  Katibu mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na ushirikiano wa Kenya Bw. Chris Kiptoo amesema mjini Nairobi kuwa, nchi hizo mbili zinafuatilia kushuka kwa biashara tangu mwaka 2015. Amesema pande mbili zimekubaliana kukutana mjini Mombasa kwa ajili ya kutafuta njia ya kuondoa vizuizi vya ushuru ambavyo vinasababisha kushuka kwa biashara.

  Habari hiyo inatolewa wiki moja baada ya Kenya na Tanzania kufanya mazungumzo ya siku tatu mjini Dar es Salaam, Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako