• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchaguzi wa marudio wahatarisha kuleta utengano kwa wanasiasa na waungaji mkono nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2017-09-13 10:10:26

  Wanasiasa wa Kenya wamekuwa wakirushiana lugha za matusi na wengine wakitishaiana. Hilo ndilo lilnalotokea katika mazingira ya kisiasa ya Kenya wakati wanasiasa wakichukua hatua zote katika kampeni zinazoendelea kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa marudio utakaofanyika Oktoba 17.

  Mahakama kuu Septemba 1 ilifuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi uliofanyika Agosti 8 na kuamuru kufanya uchaguzi wa marudio kutokana na ukiukaji wa sheria katika mchakato wa uchaguzi.

  Hivi sasa muungano wa vyama vya upinzani NASA unaoongozwa na Bw. Raila Odinga na chama cha Jubilee kinachoongozwa na rais Uhuru Kenyatta, vinashambuliana ili kuwavutia wapigaji kura kuwapigia kura.

  Rais Kenyatta alipotoa hotuba katika ufunguzi rasmi wa bunge la awamu 12, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakenya kuwa uchaguzi sio tu mashindano kati ya watu hao wawili, bali pia ni shughuli muhimu ambayo mamilioni ya wakenya kumpa madaraka kiongozi wa chaguo lao.

  Ametoa tahadhari kuwa chaguo linalofanywa na wakenya, halitakiwi kufutwa kutokana na masuala yasiyohusiana na machaguo ya watu.

  Rais Kenyatta juzi ameonya kuwa hata kama Bw. Odinga atachaguliwa katika upigaji kura wa marudio utakaofanyika Oktoba 17, chama chake cha Jubilee kitamwondoa madarakani ndani ya miezi mitatu.

  Ameeleza kuwa chama chake kinadhibiti baraza la juu na la chini la Bunge, ambacho kitaweza kumfukuza Bw Odinga na hata kinaweza kurekebisha katiba bila kushauriana na vyama vya upinzani.

  Viongozi wa kundi la NASA wameeleza hoja ya Kenyatta kama uzembe na maneno yanayoonyesha kukata tamaa. Kiongozi wa NASA Bw. Moses Wetang'ula amesema kwa niaba ya Bw Odinga kuwa ni tuhuma gani zitaletwa na rais Kenyatta dhidi ya Bw Odinga? Maneno hayo ni uzembe usiopaswa kusemwa na rais wa nchi.

  Bw Kenyatta na Bw Odinga wote wanalaumiana kwa kuimarisha siasa za utengano na ukabila, ili kuwavutia wapigaji kura wengi zaidi, huku viongozi hao wakionekana kuacha ahadi za kampeni zao na kufanya mapambano makali zaidi ya kisiasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako