• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa taifa wa China akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2017-09-13 16:21:50

    Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson mjini Washington.

    Katika mazungumzo yao, Tillerson amesema Marekani inapenda kushirikiana na China kuandaa duru ya kwanza ya mazungumzo kuhusu jamii na utamaduni na mazungumzo kuhusu utekelezaji wa sheria na usalama wa mtandao wa internet. Pia amesema Marekani inapenda kushirikiana na China katika kuimarisha ushirikiano, mawasiliano na uratibu katika masuala ya kimataifa na kikanda, na kuhakikisha ziara ya rais Donald Trump nchini China itakayofanyika baadaye mwaka huu inapata mafanikio.

    Kwa upande wake, Bw. Yang amesema China inapenda kushirikiana na Marekani na kuhakikisha ziara hiyo inafanikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako