• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa unatakiwa kushirikiana na Umoja wa Afrika ili kutatua masuala ya kimsingi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-13 16:22:05

    Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema Umoja huo unatakiwa kushirikiana zaidi na Umoja wa Afrika ili kuisaidia Afrika kutatua masuala ya kimsingi.

    Balozi Wu amesema hayo kwenye mkutano wa wazi wa uhusiano wa kiwenzi kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Amesema kuunga mkono maendeleo ya uchumi na jamii barani Afrika ni njia muhimu ya kupanua ushirikiano kati ya pande hizo mbili, pia ni njia muhimu ya kutatua msuala ya kimsingi yanayosababisha migogoro barani Afrika. Amesema Umoja wa Mataifa unatakiwa kushirikisha utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika, na ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada na uwekezaji katika sekta za afya, elimu, uchumi na mawasiliano barani Afrika, ili kuinua kiwango cha maendeleo ya uchumi na jamii katika bara hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako