• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano mkuu wa 22 wa shirika la utalii duniani la Umoja wa Mataifa wafanyika huko Chengdu

  (GMT+08:00) 2017-09-13 18:03:50

  Mkutano mkuu wa 22 wa Shirika la utalii duniani la Umoja wa Mataifa umefunguliwa leo huko Chengdu, China. Katika kipindi cha mkutano huo, idara kuu ya utalii ya China na shirika hilo wameandaa kwa pamoja mkutano wa mawaziri wa utalii wa nchi za "Ukanda mmoja na Njia moja", ambao umetoa mwito wa kuanzisha jumuiya ya ushirikiano wa utalii kati nchi na sehemu za "Ukanda mmoja na Njia moja". Vilevile kwa mujibu wa mwito wa China, umoja wa utalii duniani ulianzishwa.

  Washiriki wa mkutano watajadili mada ya utalii na nguvu ya ushindani, maendeleo endelevu ya utalii na "utalii wenye akili": Mkurugenzi wa idara kuu ya utalii ya China Bw. Li Jinzao kwenye ufunguzi wa mkutano huo amesema, nguvu ya ushindani ya utalii ya China imeongezeka na kuchukua nafasi ya 15 duniani. China itakuwa soko kubwa zaidi la utalii duniani katika karne ya 21, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya utalii wa dunia. Hasa kutokana na pendekezo la "Ukanda mmoja na Njia moja", soko la utalii litakuwa na fursa nyingi zaidi.

  Bw. Li amesema, kuhusu ushirikiano wa utalii kati ya nchi na sehemu za "Ukanda mmoja na Njia moja", China inatumai kuongeza nguvu ya kulinda usalama wa utalii, kuimarisha ujenzi wa mawasiliano ya utalii, na kurahisisha visa za utalii na kuboresha huduma za kupokea watalii. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi husika kuendeleza mistari kuu ya utalii.

  Katibu mkuu wa shirika la utalii duniani la Umoja wa Mataifa Bw. Taleb Rifal alipohojiwa amesifu sana pendekezo la China kuhusu "Ukanda mmoja na Njia moja". Amesema pendekezo hilo linaambatana na kanuni ya kunufaishana, linalounganisha pande mbalimbali.

  Katika kipindi cha mkutano huo, China iliongoza na kuanzisha umoja wa utalii duniani. Kauli mbiu ya umoja huo ni Utalii utaifanya dunia iwe nzuri zaidi. Na lengo la umoja huo ni kuhimiza maendeleo, kupunguza umaskini na kuhimiza amani kwa kupitia utalii. Umoja huo pia utahimiza mawasiliano ya kimataifa kuhusu utalii duniani, na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya utalii duniani. Kuanzishwa kwa umoja wa utalii duniani kumesifiwa na sekta ya utalii duniani. Ofisa mtendaji mkuu wa klabu ya Mediterranean kwenye kanda ya China Bw. Gino Andreetta ameeleza imani yake kuwa Umoja wa utalii duniani, utahimiza zaidi maendeleo ya utalii katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako