• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taka za kibaiolojia kuwa chanzo kipya cha nishati nchini Namibia

  (GMT+08:00) 2017-09-13 19:00:07

  Namibia ina uwezo wa kutumia tani milioni 300 za taka za kibaiolojia kuipatia nchi hiyo rasilimali ya nishati ambayo inahitajika sana duniani.

  Kiongozi wa mradi wa Shirika la Kimataifa la GIZ la Ujerumani Frank Gschwender amesema, hivi sasa Namibia inaathiriwa na uvamizi wa misitu kwa kiasi kikubwa na hiyo inaathiri takriban hekta milioni 30 za ardhi ya kilimo katika mikoa 9 kati 14 nchini humo. Ili kuunga mkono udhibiti wa misitu na utekelezaji mzuri wa matumizi ya misitu nchini humo, Makubaliano ya Awali ya mwaka mmoja yamesainiwa kati ya Benki ya Kilimo ya Namibia, Wizara ya Kilimo nchini humo, na kampuni ya GIZ katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek. Makubaliano hayo yameelekeza maeneo ya ushirikiano kama vile maendeleo ya bidhaa, kufuatilia hatari za mikopo, kubadilishana taarifa, na kusimamia na kutathmini utekelezaji wa usimamizi wa misitu na matumizi ya taka za kibaiolojia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako