• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda:Benki ya China Exim yaanza tathmini ya mradi wa SGR Uganda

  (GMT+08:00) 2017-09-13 19:08:45

  Benki ya Exim ya China imeanza tathmini ya mradi wa SGR Uganda.

  Jumatatu,Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Fedha nchini Uganda alikutana na washauri wa tathmini wa Benki ya China Exim katika ofisi yake ili kujadili kuhusu ufadhili $2.3b kwa ajili ya mradi wa reli ya SGR katika njia ya mashariki.

  Katibu wa Kudumu katika wizara ya Fedha Keith Muhakanizi amesema mradi huo umepewa kipaumbele na serikali ya Uganda,na wanataka kuuanza mapema iwezekanavyo.

  Kampuni ya ushauri inayoitwa Fourth Railway Survey & Design Institute, katika wiki tatu zijazo itajadiliana na timu ya kiufundi ya SGR Uganda,maafisa wa Fedha na Ujenzi ili kuutathmini mradi huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako