• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Benki ya AfDB yazindua mpango mpya kupiga jeki viwanda vya bidhaa za kilimo

    (GMT+08:00) 2017-09-13 19:09:16

    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imezindua mpango wa kupiga jeki viwanda vya bidhaa za kilimo kote barani Afrika.

    Mpango huu mpya utafanya AfDB kuongeza msaada wa kifedha kwa ajili ya uzalishaji mazao na kupiga jeki viwanda barani Afrika.

    Miongoni mwa mazao yatakayopewa kipaumbele zaidi ni muhogo ambao wataalamu wanasema unaweza kutumia kuzalisha ethanol kwa ajili ya matumizi ya viwandani nan a bidhaa nyengine za nyumbani.

    Mshauri wa Naibu Rais wa Benki ya AfDB Martin Fregene amesema mpango huo unalenga kusaidia uzalishaji wa muhogo na usindikaji wake viwandani ili kuwasaidia wakulima kuongeza mapato yao.

    Aidha Benki hioyo inalenga kushirikiana na wakulima wadogo zaidi ya 200,000 ili kusaidia kuboresha mazao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako