• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tiketi za awali za kombe la dunia kuanza kuuzwa leo Alhamis

  (GMT+08:00) 2017-09-14 08:25:41

  Kuelekea michuano ya fainali ya kombe la dunia nchini Urusi itakayofanyika mwakani tayari tiketi za awali zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo Alhamisi.

  Mashabiki sasa wataweza kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani 'FIFA' na tiketi zitauzwa kwa awamu mbili.

  Mchakato wa uuzwaji wa tiketi hizo utaanza leo saa 6 mchana kwa saa za Urusi. Bei za tiketi zinatarajiwa kuanzia paundi 79 kwa mechi za mzunguko wa pili hadi kufikia paundi 829 katika mchezo wa mwisho.

  Kwa mujibu wa sera za awali kuhusiana na upatikanaji wa tiketi hizo wakazi wa nchini Urusi watakuwa na bei yao maalum itakayo anzia na paundi 17.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako