Juzi kocha wa klabu ya Simba, Joseph Omog na Mshambuliaji wa klabu hiyo, Emmanuel Okwi walipata ajali ya kugongana wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, habari nzuri ni kwamba wawili hao afya zao zinaendelea vizuri kwani jana wameonekana mazoezini.
Meneja wa Simba, Cosmas Kapinga amethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa wawili hao wapo katika hali nzuri kiafya. Taarifa za awali ziliripoti kuwa wawili hao baada ya kugongana walipelekwa hospitali kwa matibabu. Klabu ya Simba ipo kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo wake wa Ligi kuu dhidi ya Mwadui FC, utakaochezwa Jumapili Septemba 17.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |