• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yasema idadi ya watalii wanapofika Kenya haijaathiriwa na wasiwasi wa kisiasa

  (GMT+08:00) 2017-09-14 09:40:22

  Wadau wa Utalii wa Kenya wamesema hali ya wasiwasi wa kisiasa inayoendelea nchini Kenya haijaathiri idadi ya wakimbizi kutoka nje wanaoingia nchini Kenya.

  Mkuu wa chama cha wafanyakazi wa hoteli na watoa chakula cha Kenya eneo la pwani Bw Sam Ikwaye, amesema kuanzia mwezi septemba eneo la pwani limekuwa na asilimia 60 ya watalii kutoka nje. Lakini amesema watalii kutoka ndani na nchi za jirani ndio wamepungua.

  Hata hivyo amesema katika mwezi Agosti watalii kutoka nje walipungua kiasi kutokana na hofu ya vurugu za kisiasa, na pia wananchi wengi wa Kenya hawakwenda kwenye mapumziko ya shule, kutokana na hofu ya uwezekano wa kutokea vurugu.

  Bw Ikwaye amesema uchaguzi wa safari hii haijaathiri vibaya sekta ya utalii ya Kenya ikilinganishwa na uchaguzi uliopita, licha ya vyombo vya habari kusema mvutano wa kisiasa unaleta madhara kwa uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako