• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa nchi za Kiarabu wakataa upigaji kura za maoni kuhusu kujitenga kwa jimbo la Wakurd

    (GMT+08:00) 2017-09-14 09:40:42

    Wizara ya mambo ya nje ya Iraq imesema kuna makubaliano miongoni mwa nchi za kiarabu kuhusu kupinga kura za maoni za Jimbo la wakurdi la Iraq kujitenga.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iraq Bw Ahmed Gamal amesema baraza la umoja wa nchi za kiarabu limepitisha kwa kauli moja azimio la kukataa kura za maoni kuhusu uhuru wa jimbo la Wakurd. Hatua hiyo inafuatiwa na hatua kama hiyo ya bunge la Iraq, lililokataa kura za maoni kwenye jimbo la Wakurd.

    Hata hivyo mwanasiasa mwandamizi wa wakurd na aliyekuwa waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw Hoyshar Zebari alisema licha ya upinzani kutoka bunge la Iraq upigaji kura utafanyika tarehe 25 Septemba kama ilivyopangwa.

    Hata hivyo uhuru wa Kurdistan unatarajiwa kupingwa na nchi mbalimbali, zikiwezo Uturuki, Iran na Syria zitakazoona hatua hivyo ni tishio la usalama, kwa kuwa zina idadi kubwa ya wakurd kwenye nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako