• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja katika kutatua suala la nyuklia la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-14 10:06:31

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw Shi Zhongjun jana mjini Vienna kwenye mkutano wa baraza la Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, alisema China inapinga kithabiti jaribio la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini tarehe 3 mwezi huu.

    Amesema China inaitaka Korea Kaskazini izingatie matakwa ya jumuiya ya kimataifa kwenye suala la kuondoa silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea, kuheshimu maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kusimamisha vitendo vya kuharibu hali ya usalama visivyolingana na maslahi ya nchi, na kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

    Bw Shi Zhongjun ameongeza kuwa vikwazo siyo njia mwafaka ya kutatua suala hilo. Amesema China itatekeleza majukumu yake na pia inazitaka pande zote husika zichukue hatua za kiujenzi ili kupunguza hali ya wasiwasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako