• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu Mkuu wa UM atangaza mipango ya mageuzi ya kitaasisi

  (GMT+08:00) 2017-09-14 10:55:15

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametangaza mipango miwili ya mageuzi inayohusiana na amani na usawa wa kijinsia.

  Bw. Guterres ametangaza uzinduzi wa kamati ya ushauri kuhusu upatanishaji kabla ya mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

  Ameongoza kuwa kamati hiyo inaundwa na watu 18 mashuhuri duniani ambao wanatarajiwa kuleta uzoefu, ustadi, ujuzi wa kina na uhusiano mpana kwa kazi hiyo muhimu sana.

  Imefahamika kuwa wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na rais Michelle Bachelet wa Chile, Bibi Graca Machel, rais wa zamani wa Nigeria Bw. Olusegun Obasanjo na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby.

  Aidha, Bw. Guterres ametangaza mkakati wa usawa wa kijinsia kwa Umoja wa Mataifa, ambao unalenga kutimiza usawa katika ngazi ya juu hadi mwaka 2021 na katika ngazi zote mwaka 2028.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako