• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yaanza kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa biometric kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao

    (GMT+08:00) 2017-09-14 18:19:35

    Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe imeanza kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa biometric, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao.

    Kwa mara ya kwanza Zimbabwe inatumia mfumo huo ili kupata idadi halisi ya wapiga kura, ikimaanisha kuwa hata wale waliojiandikisha awali wanatakiwa kujiandikisha upya. Zoezi la uandikishaji wapiga kura litaendelea mpaka Januari 15 mwakani.

    Tume hiyo inatarajia kuandikisha wapiga kura milioni 7 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka ujao, ikiwa ni ongezeko kutoka milioni 6.8 walioandikishwa katika uchaguzi wa mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako