• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasaidia kuboresha sekta ya afya nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2017-09-14 18:21:48

    Waziri wa afya nchini Uganda Bi. Ruth Aceng amesema China imekuwa muhimu katika kuboresha maendeleo ya sekta ya afya nchini humo.

    Akizungumza kwenye hafla ya kuikaribisha timu mpya ya madaktari wa China katika Hospitali ya Urafiki wa China na Uganda mjini Kampala, Bi. Aceng ameishukuru serikali ya China kwa kuendeleza uratibu, ushirikiano, na uungaji mkono katika sekta ya afya nchini Uganda, na kufanya ukarabati wa hospitali hiyo.

    Balozi wa China nchini Uganda Zheng Zhuqiang amesema, kupelekwa kwa madaktari wa China nchini Uganda imekuwa moja ya mfumo mkubwa wa ushirikiano wa tiba na afya kati ya China na nchi za Afrika.

    Timu ya kwanza ya madaktari wa China ilikwenda nchini Uganda mwaka 1983, na tangu wakati huo, wataalam 170 wa afya wa vitengo mbalimbali ikiwemo wanawake na watoto wametoa huduma nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako