• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumuiya ya kimataifa yatakiwa kuunga mkono nchi za Afrika kutatua masuala yao kwa njia ya kiafrika

  (GMT+08:00) 2017-09-14 18:24:02

  Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuunga mkono nchi za Afrika kutatua masuala yao kwa njia ya kiafrika.

  Akizungumza kwenye mkutano wa Umoja huo kuhusu hali ya Bonde la Ziwa Chad uliofanyika jana, balozi Wu amesema China inafuatilia kwa karibu hali ya bonde hilo, na inatoa pongezi kwa mafanikio ya jeshi la muungano la nchi za kanda hiyo katika mapambano dhidi ya ugaidi. Amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuunga mkono kithabiti juhudi za nchi hizo.

  Pia amesema hatua zinatakiwa kuchukuliwa ili kupunguza hali ya wasiwasi ya kibinadamu, na China imetoa msaada wa dharura wa chakula kwa nchi za kanda hiyo ikiwemo Nigeria na Chad.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako