• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wauza nyama Uganda wasaidiwa kuimarisha sekta

    (GMT+08:00) 2017-09-14 18:54:13

    Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini Uganda (UNBS) imesaini mkataba wa maelewano na chama cha wauzaji nyama ili kuimarisha ubora wa bidhaa na usalama wake.

    Mkurugenzi wa UNBS Ben Manyindo alisema pia wanalenga kusaidia wadau wa kuuza nyama kuongeza ubora kwenye bidhaa zao ili kupata pesa zaidi.

    Alisema shirika hilo litawezesha wauza nyama kuwa mizani zinazotimia ubora unaowekwa na pia kuwapa vyeti vya kuthibitisha ubora.

    Uganda imepata changamoto ya kuuza nyama kwenye soko la kimataifa kutokana na hali duni ya ubora wa bidhaa zake.

    Nchini humo kuna maduka ya nyama yapatayo 1,400 na zaidi ya mifugo 1,500 huchinjwa kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako