• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dola milioni 280 zatolewa kusaidia kilimo Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-14 18:57:09

    Kanda ya Afrika mashariki inatarajiwa kunufaika na ufadhili wa dola milioni 280 wa kilimo unaolenga familia milioni 30 katika nchi 11 za Afrika kati ya sasa na mwaka 2021.

    Ethiopia, Kenya Tanzania na Rwanda ni miongoni mwa nchi zinazopewa kipaumbele na ufadhili huo kutoka kwa sharia la ushirikiano wa mabadiliko ya kilimo barani Afrika (Piata).

    Mradi huo ambao ulizinduliwa kwenye mkutano wa mwaka hii wa shirika la AGRA ni ushirikiano kati ya wakfu wa Rockefeller, USAid na Bill & Melinda Gates.

    Kulingana na mkurugenzi mkuu wa wakfu wa Rockerfeller barani Afrika bwana Mamadou Biteye, fedha hizo zitaisaidia wakuliwa kuendesha shughuli zao kwa kutumia teknolojia ili kuzalisha chakula zaidi.

    Nchi nyingine ambazo zitanufaika na fedha hizo ni pamoja na Ghana,Mali, Burkina Faso, Malawi na Mozambique.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako