• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Namera Group of Industries yaahidi kununua pamba yote Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-09-14 18:58:00

    Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries, Hamza Pardesi ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.

    Hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2015. Pardesi ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay Dar es Salaam jana, ambaye alisema tayari serikali imeanza kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Majaliwa alimpongeza Pardesi kwa kuiunga mkono serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya Dar es Salaam.

    Inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo Kahama. Pia Waziri Mkuu alisema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbele, alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Septemba 8, mwaka huu na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako