• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kampeni ya kuimarisha ubora wa kahawa yaanza Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-09-14 19:00:42

    Halmashauri ya kuuza bidhaa za kilimo nje nchini Rwanda imeanzisha kampeni ya kitaifa ya kuhamasiha upandaji na unywaji wa kahawa.

    Kampeni hiyo ni sehemu ya siku ya kahawa nchini Rwanda mwaka 2017 na pia kupigia debe utumiaji wa bidhaa zinazozalishwandani ya nchi.

    Mkuu wa kitengo cha kahawa kwenye halmashauri hiyo Dkt. Celestin Gatarayiha, amesema wanahimiza wakulima kukumbatia kilimo bora na pia njia za kuhifadhi kahawa yao ili kuongeza ubora.

    Garayiha amesema kipaumbele ni kuhimiza watu kunywa kahawa na kuongeza ubora ili kupata bei zuri.

    Kahawa imechangia asilimia 24 ya mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo ndani ya miaka 10 iliopita na hutegemewa na zaidi ya wakulima 400,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako