• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Alan Ruschel aliyenusurika kwenye ajali ya ndege acheza mechi yake ya kwanza

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:46:58

    Mchezaji wa klabu ya soka ya Chapacoense ya Brazil Alan Ruschel ambaye alinusurika kwenye ajali ya ndege mwaka jana amecheza mechi yake ya kwanza ya ushindani usiku wa kuamkia jana. Alan alinusurika pamoja na wenzake wawili ambao ni Neto na Jackson Follman huku abiria wengine 71 wakipoteza maisha katika ajali hiyo.

    Mlinzi huyo wa kati amecheza dakika 73 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa Amerika Kusini dhidi ya Flamengo ambapo timu hizo zimetoka sare tasa.

    Ruschel amekuwa akitokwa na machozi mara zote anapoingia uwanjani ambapo mara ya kwanza alicheza dakika chache kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Barcelona. Flamengo na Chapacoense zitarejeana tena Septemba 20 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako