• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha Wu Jingui asema Carlos Tevez hataichezea Shanghai Shenhua hadi apugue unene

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:48:33

    Mshambuliaji wa Argentina Carlos Tevez ameambiwa na mkufunzi mpya wa klabu yake ya Shanghai Shenhua ya hapa China Wu Jingui kwamba ni mnene na hatachezea timu hiyo hadi apunguze uzani na kuwa sawa kucheza.

    Tevez, 33, ambaye anaaminika kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani, amefunga mabao mawili pekee katika mechi 12 tangu alipoanza kuwachezea mwezi Machi. Wu, aliyechukua usukani katika klabu hiyo baada ya Gus Poyet kujiuzulu Jumatatu, pia alimkosoa kiungo wa kati Fredy Guarin. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Manchester City alihamia Shanghai kutoka Boca Juniors.

    Hata hivyo alikosa karibu nusu ya mechi za klabu hiyo msimu huu kutokana na majeraha. Alirejea China hivi majuzi baada ya ziara ya wiki mbili nchini Argentina ambako alikuwa ameenda kutibiwa tatizo la misuli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako