• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OCHA yasema wakimbizi laki 1.82 wameingia nchini Sudan mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:48:47

    Shirika la uratibu wa mambo ya kibinadamu la umoja wa mataifa OCHA, limesema wakimbizi laki 1.82 wa Sudan Kusini wameingia nchini Sudan mwaka huu.

    Shirika hilo limesema wakimbizi laki 4.6 wa Sudan Kusini wanaokimbia njaa na vurugu wameingia nchini Sudan Kusini tangu mwaka 2013, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto. Wakimbizi wengine 241 wanawasili nchini Sudan kila siku.

    Mapema umoja wa mataifa ulisema watu milioni 7.5 kati ya watu milioni 12.5 wa Sudan Kusini wanahitaji msaada wa kibinadamu, na wengine milioni 4.9 wanasumbuliwa na usalama wa chakula, kukosa makazi na kudorora kwa uchumi.

    Kutokana na maswala ya usalama na njaa kwenye eneo kubwa la Sudan Kusini idadi ya wakimbizi wanaoingia Sudan inatarajiwa kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako