• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la upinzani la SPLM tawi la Kaskazini limesema liko tayari kuzuia shambulizi la jeshi la serikali

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:51:12

    Kundi la upinzani la SPLM tawi la kaskazini limesema liko tayari kuzuia shambulizi lolote litakalofanywa na majeshi ya serikali, kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo kwenye jimbo la Blue Nile.

    Msemaji wa kundi hilo Bw Mubarak Ardol amesema wameona jeshi la serikali yakisogea kutoka boma la Damazin na kuelekea kwenye milima ya Angsana kwenye maeneo ya kundi la SPLM. Amesema majeshi hayo yamesogea karibu hadi karibu na mstari wao wa mbele, na wanaweza kushambulia wakati wowote.

    Kundi la SPLM Tawi la Kaskazini limekuwa linapambana na majeshi ya serikali tangu mwaka 2011 katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile, na katika siku za karibuni limekuwa likisumbuliwa na mgogoro wa ndani, uliosababishwa na kuondolewa madarakani kwa kiongozi wake mkuu, na nafasi yake kuchukuliwa na makamu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako