• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Ethiopia zinaweza kuongoza kuvutia uwekezaji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:51:33

    Ripoti iliyotolewa na shirika la ushauri kuhusu hatari za uchumi, Control Risks, inaonyesha kuwa Kenya na Ethiopia zinaweza kuwapita miamba wa uchumi barani Afrika Nigeria, Afrika Kusini na Misri kwenye kuvutia uwekezaji.

    Ripoti hiyo iliyotolewa mjini Johannesburg, inasema licha ya kuwa Nigeria na Afrika Kusini zimefufuka kiuchumi, lakini bado zinakabiliwa na hatari.

    Ethiopia ambayo ni nchi yenye ongezeko lenye kasi zaidi la uchumi barani Afrika, imezitangulia nchi zote za Afrika, ambapo mwaka jana ilivutia vitega uchumi vyenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.2.

    Kenya ina nafasi nzuri kwa kuwa imepiga hatua kwenye kuwa na nguvu kazi yenye elimu na ubunifu kwenye sekta ya huduma, serikali kuendelea kuwekeza kwenye miundo mbinu, na kuimarisha mafungamano na nchi nyingine wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuifanya nchi hiyo iwe mlango kwa wawekezaji kuingia kwenye soko kubwa la Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako