• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafadhiliwa dola milioni 66 na Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:52:00

    Serikali ya Tanzania imepokea dola milioni 66 za kimarekani kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha vituo 100 vya afya nchini humo.

    Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dk. Hamisi Kigwangala amesema msaada huo utawawezesha madaktari kutoa huduma kwa wajawazito kabla ya kujifungua. Amesema serikali imeanza kutoa fedha kwa wilaya zote zilizolengwa ili kuongeza huduma za afya.

    Pia amesema hatua hiyo ya Benki ya Dunia itanufaisha Mpango wa Afya wa nchi hiyo, unaoshughulikia usambazaji wa vifaa muhimu vya uzazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako