• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Iraq lamtimua mkuu wa mkoa wa Kirkuk

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:52:38

    Bunge la Iraq jana limepitisha azimio la kumtimua mkuu wa mkoa wa Kirkuk Bw Najemdin Karim, ambaye ameunga mkono upigaji kura za maoni wa jimbo la wakurd.

    Habari zinasema mapema jana ofisi ya spika wa bunge la Iraq ilitangaza kuwa waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abad aliwasilisha ombi kwenye bunge la Iraq akitaka kumtimua Bw Karim, na wabunge wengi walioshiriki kwenye mkutano wamekubali ombi hilo.

    Chama cha Kikurdi PUK kinachoongozwa na waziri mkuu wa zamani wa Iraq Bw Jalal Talabani kimepinga vikali kupitishwa kwa uamuzi huo.

    Mwezi Juni mwaka huu, jimbo la wakurd lilitangaza kuwa upigaji kura za maoni kuhusu kujitenga na Iraq utafanyika tarehe 25 mwezi huu, uamuzi ambao umepingwa na serikali kuu ya Iraq, Uturuki na Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako