• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:53:02

    Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kuyaweka mashirika na watu 11 kwenye orodha ya vikwazo, kutokana na kuunga mkono mpango wa Iran wa kuendeleza makombora na kufanya shambulizi la mtandao wa internet dhidi ya Marekani.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha ya Marekani imesema idara ya usimamizi wa mali za nje itaweka vikwazo dhidi ya mashirika na watu hao 11, ambao mali zao nchini Marekani zitazuiliwa, na raia wa Marekani pia hawaruhusiwi kufanya biashara nao.

    Waziri wa fedha wa Marekani Bw Steven Mnuchin amesema wizara yake itaendelea kuchukua hatua kali kujibu uchokozi wa Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako