• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria lasonga mbele kuelekea Deir al-Zour na kutwaa maeneo mapya

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:56:17

    Shirika la uangalizi wa haki za kibinadamu la Syria limesema, jeshi la serikali ya Syria limepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya kundi la IS mjini Deir al-Zour, huku likitwaa vituo vya kijeshi ambavyo lilipoteza mwaka jana.

    Shirika hilo limesema jeshi hilo limetwaa wilaya ya Bughailiyeh iliyoko katika kitongoji cha mji huo pamoja na vituo vya kijeshi lilivyopoteza katika mapigano na kundi la IS mwaka jana.

    Shirika hilo pia limesema, jeshi la serikali ya Syria na wenzi wake wanajaribu kuzingira sehemu zinazodhibitiwa na kundi la IS mjini humo.

    Kufuatia shambulizi la wiki iliyopita, jeshi hilo limesonga mbele na kutwaa asilimia 64 ya maeneo ya Deir al-Zour, huku kundi la IS likidhibiti asilimia 36 ya mji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako