• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya sita ya mazungumzo ya Syria yafanyika Astana

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:59:48

    Habari kutoka wizara ya mambo ya nje ya Kazakhstan zinasema, duru ya sita ya mazungumzo kuhusu suala la Syria imefanyika huko Astana, Kazakhstan, na kuhudhuriwa na ujumbe wa serikali ya Syria na makundi ya upinzani.

    Habari zinasema mazungumzo hayo yanaendelea leo, ambapo pande mbalimbali zitajadiliana ipasavyo kuhusu nyaraka mbalimbali, ili kutunga kanuni ya operesheni ya kikosi kinachosimamia usitishaji vita katika jimbo la Idlib, na kuthibitisha nani atashiriki kwenye kikosi hicho.

    Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan amesema, chini ya mazungumzo ya Astana, baadhi ya sehemu ya Syria zimesimamisha vita na pande mbalimbali zimesaini makubaliano ya kusitisha vita na kuanzisha maeneo matatu yasiyo na mapambano, duru mpya ya mazungumzo itajadili kuanzisha eneo jipya lisilo na mapambano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako