• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kimataifa ya nne ya helikopta nchini China yavutia wabiashara wengi wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-09-15 16:41:08

    Maonesho ya kimataifa ya nne ya helikopta nchini China yamefanyika jana huko Tianjin, na kuvutia wafanyabiashara wengi duniani.

    Mfanyakazi wa kituo cha huduma za matibabu dharura cha Beijing Bw. Zhang Xuetian ameshiriki kwenye maonesho hayo. Amemwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, mustakabali wa huduma za matibabu kwa helikopta nchini China ni mzuri. Amesema, hivi sasa huduma za matibabu kwa helikopta zinakaribishwa na wachina wengi zaidi, mahitaji ya helikopta yamekuwa makubwa, na kituo cha huduma za matibabu dharura cha Beijing kitaagiza baadhi ya helikopta kwa matumizi ya ukoaji wa matibabu.

    Mbali na huduma za matibabu, helikopta pia zinatumika katika usafirishaji wa mafuta kati ya bahari na nchi kavu, ukaguzi wa nyaya za umeme, uchimbaji wa madini, na kukabiliana na moto. Hadi kufikia tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu, idadi ya helikopta zinazotumia kiraia nchini China ilikuwa imefikia 900. Takwimu zilizotolewa na kampuni ya Airbus zinaonesha kuwa, hivi sasa China inakadiriwa kuagiza helikopta 100 kila mwaka, na kuwa soko kubwa zaidi duniani kwa kampuni hiyo, baada ya Marekani.

    Soko kubwa la China limevutia wafanyabiashara wengi wa kimataifa. Kampuni zaidi ya 400 kutoka nchi na sehemu 22 zimeshiriki kwenye maonesho hayo. Licha ya hayo, kampuni maarufu zikiwemo Airbus, Bell na Leonardo zimefikia makubaliano na upande wa China kuhusu uagizaji wa helikopta zaidi ya 500, ambazo zitakabidhiwa kwa China ndani ya miaka 10 ijayo. Kampuni ya Airbus tu imeagizwa helikopta 50 na China.

    Bw. Glen Giammalva kutoka Marekani sasa anazisaidia kampuni za China kutoa mafunzo kwa marubani. Anaona soko linalokua kwa kasi litaleta changamoto kubwa kwa China kuwaandaa wafanyakazi husika. Amesema kuna kazi nyingi za mafunzo, si kama tu kwa marubani na mafundi, bali pia kwa meneja na wamiliki wa kampuni za helikopta.

    Meneja mkuu wa kampuni ya Rockwell Collins ya Marekani nchini China Bw. He Weichang amesema, ili kukabiliana na changamoto hizo, China inaweza kufanya ushirikiano na kampuni za Ulaya na Marekani, na kuiga teknolojia na uzoefu wao.

    Bw. He amesema, China inaweza kufanya ushirikiano na kampuni za kigeni zinazotengeneza helikopta kwenye teknolojia zinazotumika kiraia, hii itainua kwa kasi kiwango cha sekta ya helikopta nchini China na kufikia kiwango cha dunia. Vilevile amesema kampuni yake na wenzi wake wa China wanabadilishana uzoefu, kwani wenzi wake wanaelewa sana soko la helikopta la China, na kampuni yake ina ujuzi zaidi wa teknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako