Makao makuu ya jeshi la Marekani ya kanda ya pasifiki limesema, jana usiku Korea Kaskazini ilirusha makombora yaliyopita anga ya Japan na kuanguka katika bahari ya Pasifiki.
Serikali ya Japan ilithibitisha taarifa hiyo na kulaani vikali kitendo hicho cha Korea Kaskazini.
Wakati huohuo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema China inapinga jaribio la kombola lililofanywa na Korea Kaskazini ambalo limekwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |