• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Nairobi hadi Mombasa latarajiwa kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-09-15 18:19:29

    Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Nairobi hadi Mombasa linatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwaka huu huku asilimia 94 ya ujenzi ukiwa umekamilika. Kampuni inayojenga bomba hilo Zakhem International Construction imesema mradi huo ulichelewa kiasi kutokana na kubadili ramani jambo ambalo lilipelekea kucheleweshwa kwa manunuzi ya vifaa vinavyohitajika. Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya ujenzi amesema wako katika hatua ya mwisho . Pindi mradio huo utakapokamilika unatarajiwa kupunguza gharama za kurekebisha barabara.Wakati huo huo majaribio ya treni ya mizigo ya SGR ambayo yalikuwa yamepangwa kufanywa mwezi ujao huenda yakahahirishwa kutokana na marudio ya uchaguzi Octoba 17.Waziri wa uchukuzi Bw James Macharia amesema ijapokuwa mkandarasi mchina amejitolea kuhakikisha kila kitu kinafanywa kwa wakati wamelazimika kuhahirisha kutokana na uwezekano wa mazingira mabaya ya kisiasa huenda yakashuhudiwa wakati wa uchaguzi huo mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako